Dozi milioni 10 za malaria zimepelekwa Afrika
23 Januari 2025Matangazo
Gavi amesema zaidi ya dozi milioni 9.8 zimetolewa, na kusema angalau watoto milioni tano wamepata ulinzi wa kutosha.
Soma pia: Ugonjwa wa Malaria waongezeka kwa kasi Rwanda
Kulingana na Gavi, programu hiyo inalenga kutoa chanjo nne kwa kila mtoto na kusisitiza kwamba kila mara ulilenga kuwafikia watu wanaokabiliwa na kitisho zaidi katika kila nchi.
Shirika la Afya ulimwenguni, WHO limesema ugonjwa wa Malaria huua karibu watu 600,000 kwa mwaka, wengi zaidi kutoka Afrika, na waathirika wakubwa wakiwa ni watoto.