1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la M23 wataka wakimbizi warudi makwao Rutshuru.

21 Novemba 2023

Kundi la waasi wa M23 limetaka wakimbizi wa vita walioko katika makambi ya wakimbizi karibu na mji wa Goma waruhusiwe kurudi nyumbani katika eneo la Rutshuru.

https://p.dw.com/p/4ZG4p
DR Kongo Ein M23-Rebellen
Wapigaji wa kundi la M23 wakiwa katika operesheni zao huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Picha: GLODY MURHABAZI/AFP via Getty Images

Hata hivyo jamii ya kiraia ya Rutshuru na baadhi ya wadau wa kisiasa wamepinga wazo hilo kwa sababu ya kuzorota kwa usalama katika maeneo yanayoshikiliwa na M23.

Akizungumza katika mkutano ulioitishwa mwishini mwa wiki, mkuu wa M23, Bertrand Bisimwa, ameeleza haja wakimbizi kurudi makwao kutokana na hali aliyoiita kuwa duni pamoja na mazingira mabaya ya maisha ya wakimbizi katika makambi karibu na Goma.

Kauli ya kundi la M23 katika kupanua wigo wa amani ya DRC

DR Kongo Ein M23-Rebellen
Mpiganaji wa kundi la M23 akiwa eneo la Kibumba, huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Picha: GLODY MURHABAZI/AFP via Getty Images

Kwa mujibu wake, lengo la M23 ni kukuza maisha ya amani nchini Congo, kama ilivyo kwa nchi jirani Rwanda. Zaidi anasdema "Tunataka kila raia wa Congo aishi vizuri nyumbani kwake, kama ilivyo kwa Wanyrwanda wanavyoishi nchini mwao. Wakimbizi wetu wamegeuzwa biashara kwa bahati mbaya. Wanatumika na asaszi za kiraia na serikali. Kila siku wapo katika kilio."

Aidha Bisimwa aliendelea kusema wamewapokea wengi ambao wamerejea katika eneo lao. Na walipofika, walichukua jukumu la kuwajibika kwao. Wanapata maisha bora na kulima mashamba yao. Na wamejifunza kuwa wengine hata wanabakwa na kuuawa katika makambi ya wakimbizi. Kile wanachokifanya ni kuwahamasisha kurudi nyumbani kwao.

Wakimbizi wa vita wanateseka zaidi ya wale wanaosalia vijijini

Kuna wadau wa kisiasa wa eneo la Rutshuru wanaosema hawaegemei upande wowote kuhusu wito huu wa M23. Hope Sabini, mbunge wa Rutshuru, anaamini kwamba wale waliokimbia vita wanapitia mateso mabaya zaidi kuliko wale waliobaki vijijini mwao.

Shirika ya kiraia ya Rutshuru linasema hawalikubali wazo hili. Kulingana na Jean Claude Bambaze, mkuu wa kundi hilo la kiraia, ukosefu wa usalama unaongezeka katika maeneo yanayoshikiliwa na M23. Hii inaendelea kusababisha hasara ya maisha na pia, utoaji wa fidia usiokuwa na maana ambao unaendelea kuiharibu jamii katika vijiji ambavyo usalama wao hauhakikishwi.

Soma zaidi:Wapinzani DRC wafanya mazungumzo Afrika Kusini

Swala la kurudi makwao wakimbizi wa vita katika eneo la Rutshuru bado ni suala linalozua mjadala mkali. Huku M23 wakisisitiza umuhimu wa hatua hii, jamii ya kiraia, baadhi ya wadau wa kisiasa, na watu wa eneo hilo wanatoa wasiwasi muhimu. Kutatua hali hii ngumu inaonekana kutegemea siyo tu kwa M23 bali pia kwa ushirikiano na mashirika ya kimataifa kama HCR kuhakikisha usalama wa jamii zinazohusika.