Matangazo
Duru zinasema mkutano huo uliopangwa kufanyika siku ya Jumatatu mjini Doha, chini ya upatanishi wa taifa hilo la Ghuba umefutwa dakika za mwisho baada ya Rais wa Kongo, Felix Tshisekedi kutofanya safari kwenda nchini Qatar. Sababu gani hasa huenda zimechochea msimamo huo wa serikali ya Kongo? Swali hilo na mengine Rashid Chilumba amemuuliza Ali Mali, mchambuzi wa siasa za Maziwa Makuu.