1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Droni za Urusi zatishia usalama wa bandari za Danube

16 Agosti 2023

Jeshi la Ukraine limesema hii leo kwamba idadi kubwa ya droni za Urusi zimeingia katika mlango wa ziwa Danube, zikiwa zinaelekea kwenye bandari ya ziwa Izmail karibu na mpaka wa Romania.

https://p.dw.com/p/4VE6f
Duka kuu lililoharibiwa na shambulio la droni za Urusi, Odessa
Duka kuu lililoharibiwa na shambulio la droni za Urusi, OdessaPicha: OLEKSANDR GIMANOV/AFP/Getty Images

Makundi ya mitandao ya kijamii yaliripoti kusikia mifumo ya ulinzi wa angani ilifyatua risasi katika eneo hilo karibu na bandari mbili za Danube, za Izmail na Reni.

Gavana wa mkoa wa kusini wa Odessa, Oleh Kiper aliwaomba wakazi wa wilaya ya Izmail kujificha majira ya saa 1.30 za usiku na baada ya saa moja, aliiondoa tahadhari ya uvamizi wa angani.

Bandari za Danube nchini Ukraine zinatumika kusafirisha karibu robo ya nafaka zinazopelekwa nje ya nchi hiyo kabla ya Urusi kujiondoa kwenye makubaliano ya kusafirisha nafaka kupitia Bahari Nyeusi.