Droni za Urusi zauwa 4, zajeruhi 12 Kharkiv
4 Aprili 2024Matangazo
Gavana Oleh Syniehubov na Meya Ihor Terekhov walitangaza kupitia mtandao wa kijamii wa Telegram asubuhi ya Alkhamis (Aprili 4) kwamba raia mmoja na maafisa watatu wa uokoaji ni miongoni mwa waliouliwa katika eneo hilo lenye makaazi ya raia.
Kwa mujibu wa maafisa, majengo kadhaa yaliharibiwa likiwemo jengo la ghorofa nyingi lenye makaazi ya watu.
Soma zaidi: Urusi yaionya Ufaransa fikra ya kupeleka wanajeshi Ukraine
Kati ya droni 20 ambazo Urusi ilizitumia kuishambulia Ukraine usiku wa kuamkia Alkhamis, 15 zilielekezwa katika mji wa Kharkiv.
Mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine ulifanikiwa kuzidunguwa baadhi ya droni hizo.