1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Droo ya AFCON 2017 yaandaliwa

20 Oktoba 2016

Cote d'Ivoire itatoana jasho na aliyekuwa kocha wake Mfaransa Herve Renard baada ya kutumbukizwa katika kundi moja na Morocco katika droo iliyoandaliwa jana ya michuano ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika

https://p.dw.com/p/2RUWI
Afrika Cup Sambia gegen Elfenbeinküste Trainer Herve Renard
Picha: picture-alliance/dpa

Renard aliiongoza The Elephants wa Cote d'Ivoire katika fainali za kombe hilo mwaka 2015 na sasa anaelekea tena Gabon lakini mara hii akiwa na jeshi la nchi tofauti kabisa. Wenyeji Gabon watafungua dimba hilo mnamo Januari 14, huku mchezo wa fainali ukipangwa kuwa Februari 5.

Droo ya makundi AFCON 2017

Kundi A

Gabon, Burkina Faso, Cameroon, Guinea Bissau

Kundi B

Algeria, Tunisia, Senegal, Zimbabwe

Kundi C

Cote d'Ivoire, DR Congo, Morocco, Togo

Kundi D

Ghana, Mali, Misri, Uganda

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Grace Kabogo