DW yafungiwa nchini Uturuki
1 Julai 2022Mwenyekiti wa mamlaka hiyo Ilhan Tasci kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter usiku wa kuamkia leo kwamba tovuti za mashirika hayo yote mawili zimefungwa kufuatia amri ya mahakama iliyotokana na ombi la mamlaka hiyo ya Uturuki.
Tasci amesema mashirika yote mawili yalikuwa hayajawasilisha maombi ya vibali vya kufanyia kazi nchini humo.
DW imethibitisha kwamba tovuti zake zote za lugha 32 zilikuwa hazifanyi kazi kaunzia usiku wa jana nchini Uturuki huku VOA nayo ikithibitisha kufungiwa kwa tovuti yake.
DW na mashirika mengine ya habari ya kimataifa nchini Uturuki yamekuwa yakipokea vitisho tangu Februari, wakati ambapo shirika hilo linalosimamia vyombo vya habari Uturuki lilipoyataka mashirika hayo kuwasilisha maombi ya leseni kwa huduma zake zinazohitajika sana.