1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

ECOWAS yatafakari hatua zinazofuata mzozo wa Niger

12 Agosti 2023

Viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi wanatakafari hatua za kuchukua katika wakati wamedhamiria kuulazimisha utawala mpya wa kijeshi nchini Niger kuachia madaraka na kurejesha serikali ya kidemokrasia.

https://p.dw.com/p/4V5og
Nigeria Abuja | ECOWAS-Treffen zu Niger-Putsch
Viongozi wa Jumuiya ya ECOWASPicha: Gbemiga Olamikan/AP/picture alliance

Hata hivyo mipango yao ikiwemo tangazo la kuunda kikosi cha kijeshi kitakachotumwa nchini Niger huenda inatiwa kiwingu na uungaji mkono wa umma unaoongozeka kwa majenerali walioipindua serikali.

Hapo jana maelfu ya watu walimiminika kwenye mitaa ya mji mkuu wa Niger, Niamey kukosoa maazimio ya Jumuiya ya Kikanda ya ECOWAS ya kutaka kuingilia kati kijeshi nchini humo.

Hadi sasa bado ECOWAS haijafafanuwa undani wa kikosi hicho wala ratiba ya hatua zake, huku viongozi wa kanda hiyo wakisisitiza kuwa bado wanataka suluhisho la amani.

Hapo jana mkutano muhimu wa kijeshi uliopangwa na jumuiya hiyo kujadili mapendekezo ya kuushughulikia mzozo wa Niger uliahirishwakwa muda usiojulikana.