1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ecuador yapiga kura katika uchaguzi wa rais

20 Agosti 2023

Raia wa Ecuador wanapiga kura katika uchaguzi wa rais uliochafuliwa na mauaji ya mgombea mkuu na ambayo yanadhihirisha ukubwa wa tatizo la machafuko yanayoshuhudiwa.

https://p.dw.com/p/4VMu8
Ecuador I uchaguzi wa urais, Quito
wanajeshi wakipanga masanduku ya kupigia kura mjini Quito, Ecuador wakati wa uchaguzi wa urais.Picha: Henry Romero/REUTERS

Wagombea wanane wa urais wamezipa kipau mbele ahadi za kukabiliana na uhalifu wa kupangwa, wakati wote wakifanya kampeni wakiwa na vizibao vya kuzuia risasi katika taifa hilo lililowahi kuwa na amani na linalojikuta katika biashara ya dawa za kulevya duniani.

Mkuu wa genge la uhalifu anayehusishwa na kuuliwa kwa mgombea urais Ecuador ahamishiwa jela nyingine

Taifa hilo dogo la Amerika Kusini katika miaka ya karibuni limekuwa kitovu cha walanguzi wa kigeni wa dawa za kulevya wanaotaka kusafirisha cocaine na kusababisha vita vikali kati ya magenge hasimu nchini humo.

Marekani kusaidia uchunguzi mauaji ya mgombea urais Ecuador

Kulikuwa na mauaji kadhaa ya kisiasa kabla ya uchaguzi huo, huku mauaji ya mgombea maarufu wa urais Fernando Villavicencio, zikiwa zimesalia siku 11 tu kwa kura hiyo, yakidhihirisha changamoto zinazoikumba nchi hiyo.