Bwawa la Kakhovka lasababisha mafuriko makubwa
8 Juni 2023Matangazo
Gavana wa mkoa huo, Oleksandr Prokudin amesema asilimia 86 ya sehemu iliyoathiriwa iko chini ya udhibiti wa Urusi, kwenye ukingo wa kushoto wa mto Dnipro. Kina cha wastani cha maji ya mafuriko hayo kilikuwa cha mita 5.61 mkoani Kherson siku ya Alhamis. Mwanaharakati wa mazingira kutoka shirika la Greenpeace Denys Tsutsaiev amesema hali hiyo inatishia baioanuai.
Watu wahama eneo la mafuriko
Kupitia mkanda wa video, gavana wa Kherson Oleksandr Produkin amesema watu wapatao 2000 walikuwa wameondoka katika eneo la mafuriko hadi leo asubuhi, na kuongeza kuwa licha ya kitisho cha mashambulizi ya Urusi, shughuli za kuwahamisha watu zinaendelea.