1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

England iko tayari kuweka historia

11 Julai 2021

Timu ya taifa ya England inatarajia kusajili historia usiku wa Jumapili katika fainali ya michuano ya EURO 2020 wakipania kufikia kikomo cha ukame wa kombe wa miaka 55 lakini Italy inalenga kusitisha azma hiyo.

https://p.dw.com/p/3wJpw
Fußball EM | England v Dänemark | Fans
Picha: Frank Hoermann/SVEN SIMON/imago images

Kocha Gareth Southgate imeiwakilisha vyema England kwa kutinga fainali ya kwanza katika michuano ya Ulaya, na kuiweka hatua moja kabla kushinda taji la kwanza tangu waliposhinda kombe la Dunia mwaka 1966.

England imefuzu kwa fainali ya kwanza ya mashindano makubwa tangu 1966 na itamenyana na Italia. Soma Fainali EURO 2020: Vita vitakuwa kati ya manahodha

Fainali hii katika uga wa Wembley huko London ni kilele cha Mashindano ya Ulaya yaliyodumu kwa mwezi mmoja ambayo, kwa mara ya kwanza, yamefanyika sio katika nchi moja mwenyeji lakini katika miji 11 barani Ulaya.

Bildkombo Harry Kane - Giorgio Chiellini
Harry Kane - Giorgio Chiellini

Burudani viwanjani

Michuani hii imekuwa yakusisimua, kuanzia kubanduliwa kwa mabingwa watetezi wa kombe hilo Ureno, kuondolewa kwa mabingwa wa ulimwengu Ufaransa pamoja na kikosi cha Joachim Löw Ujerumani. Soma Ufaransa yaondolewa Euro 2020

Kulisajiliwa mabao maridadi, kama vile la Paul Pogba wa Ufaransa dhidi ya Uswizi bila kusahau goli la  Mikkel Damsgaard kwa Denmark dhidi ya England, pia kumekuwa na makosa ya walindaji lango kama vile Martin Dubravka wa Slovakia na Unai Simon wa Uhispania.

Lakini pia kulikuwa na mkasa katika mechi ya ufunguzi wakati mchezaji wa Denmark Christian Eriksen alipata mshutuko wa moyo kiwanjani katika mechi dhidi ya Finland.

Fußball EM | Frankreich - Deutschland
Picha: Federico Gambarini/dpa/picture alliance

Mashabiki watakuwepo uwanjani

Lakini kwa usiku wa leo macho yote na masikio ya mashabiki wa soka yataelekea katika uwanja wa Wembley, kwa mechi kati ya Italy na England. Soma Mashabiki uwanjani Wembley na virusi vya corona

Kikosi cha England kimepokea ujumbe wa heri njema kutoka kwa Malkia Elizabeth II, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na hata muigizaji wa Hollywood Tom Cruise.

Italy chini ya kocha Roberto Mancini hawajafungwa katika mechi 33 na bila shaka imekuwa timu bora katika mashindano haya ikiingia kwenye hatua ya makundi na rekodi nzuri kabla ya kuitoa Austria, Ubelgiji iliyo juu na Uhispania kufikia fainali.

Mabingwa mara nne wa ulimwengu Italy mara ya mwisho walishinda mashindano ya Ulaya mnamo 1968, kisha wakipoteza fainali zao mbili za mwaka 2002 na 2012.

 

AFPE/ https://p.dw.com/p/3wJ7i