1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

England yaibwaga Czech, Croatia yaiondoa Scotlan

Yusra Buwayhid
23 Juni 2021

England imekamata nafasi ya juu katika Kundi D baada ya kupata ushidi wa bao 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech katika mechi iliyochezwa mjini London hapo jana na kufuzu 16 bora kwa shangwe nyingi.

https://p.dw.com/p/3vPCa
Euro 2020 | England - Tschechien Republik Sterling
Picha: Laurence Griffiths/Getty Images

Raheem Sterling ndiye aliyeipatia England ushindi huo kwa goli pekee lilofungwa kwenye mechi hiyo kwa usaidizi wa Jack Grealish. Timu hiyo ya Uingereza itabakia mjini London kwa sasa hadi Jumanne itakapovaana na timu inayoshika nafasi ya pili kwenye Kundi F, ikimaanisha huwenda wakakabiliana na mabingwa wa dunia Ufaransa, Mabingwa watetezi wa michuano hiyo ya mataifa ya Ulaya timu ya taifa ya Ureno au Ujerumani.

Akizungumzia timu watakayokabiliana nayo wiki ijayo, Sterling amekiambia kituo cha televisheni cha Uingereza ITV kwamba wakati mwingine lazima ukabiliane na timu bora. Na hivyo ndivyo unavyoweza kujipima uwezo wako.

Wacheki walimaliza katika nafasi ya tatu na kufuzu kuingia kwenye raundi ya mtoano licha ya kuzidiwa kwa kwa mabao yaliyofungwa na Croatia, ambayo alishinda Scotland 3-1. Waskochi, wakishika nafasi ya nne, wameyaagaa mashindano hayo na kurudi nyumbani.

Kuna msemo usemao, kutia goli wavuni ni kitu kinachohukua sekunde tu, lakini bahati mbaya kwa timu ya Scotland iliwachukua takriban masaa matatu na dakika 42 kuoona wavu ya goli ulipo katika michuano hiyo ya mataifa ya Ulaya.

Euro 2020 | Kroatien Schottland Perisic  Jubel
Modric alikuwa moto wa kuotea mbali uwanjaniPicha: Paul Ellis/REUTERS

Magoli ndiyo sarafu yenye thamani zaidi kwenye mpira wa miguu na licha ya juhudi zote za Scotland, ustahimilivu, uchokozi wao wote, walishindwa kuweka mpira kwenye wavu ili kuiokoa timu yao.

Walikuja kwenye mchezo wao huo wa mwisho wakiwa timu pekee ambayo bado haijafunga bao hata moja kwenye michuano hiyo ya Euro 2020,  na wakati mchezaji Callum McGregor aliwapa matumaini katika kipindi cha kwanza kuwa huenda wagefikia hatua ya mtoano, walishindwa kufanikisha hilo katika kipindi kilichobakia cha mchuano huo.

Baada ya kuambulia matupu katika mechi yao ya ufunguzi kwa kupigwa mabao 2-0 na Jamhuri ya Czech na baadae kutoka sare na Uingerea kwenye uwanja wa Wembley, Scotland wanahesabiwa kuwa ni timu ambayo haijawahi kufikia hatua ya mtoano kwenye mashindano makubwa ikiwa ni mara nane kwenye michuano ya Kombe la Dunia na mara tatu kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya.

Meneja wa timu ya Scotland Steve Clarke amesema hilo linatokana na ukosefu wa uzoefu wa kucheza kwenye mashindano makubwa.

Clarke ameongeza kwamba walikabiliana dhidi ya timu ambayo ni uzoefu mkubwa wa kucheza kwenye mashindano ya aina hiyo, na hivyo ndio maana wao wanarudi nyumbani na Croatia inabakia kwenye michuano hio.

Hii leo Sweden itakuwa na miadi na Poland na Slovakia nayo ikikipiga na Uhispania.

Vyanzo: dpa, rtre