1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ennahda yasema iko tayari kutoa tahfifu Tunisia

22 Agosti 2013

Chama cha Kiislamu kinachotawala nchini Tunisia kimeashiria kuwa tayari kujadiliana na upinzani kuhusu kuundwa kwa serikali isiyo ya wanasiasa, ili kukomesha mgogoro wa kisiasa uliyodumu kwa mwezi mmoja sasa.

https://p.dw.com/p/19Ule
Rached Ghannouchi, leader of the Islamist Ennahda movement, speaks during a news conference in Tunis August 15, 2013. The chairman of Tunisia's ruling Islamist party rejected on Thursday opposition demands for a non-party government, saying this could not steer the country through "the delicate situation" it is in. Ghannouchi said he would accept the creation of a government of national unity, but only provided all political parties are represented. REUTERS/ Zoubeir Souissi (TUNISIA - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Rached Ghannouchi Ennahda Partei TunesienPicha: REUTERS

Chama cha Kiislamu kinachotawala nchini Tunisia kimeashiria kuwa tayari kujadiliana na upinzani kuhusu kuundwa kwa serikali isiyo ya wanasiasa, ili kukomesha mgogoro wa kisiasa uliyodumu kwa mwezi mmoja sasa.

Tangazo la kile ambacho kinaweza kuwa tahfifu muhimu ambayo Ennahda imepinga hadi wakati huu, lilifuatia mkutano wa mwenyekiti wa chama hicho Rachid Ghanouchi, na Haoucine Abassi, katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi chenye nguvu UGTT, ambacho kimechukua jukumu la upatanishi katika makundi hasimu. "Vuguvugu la Ennahda limekubaliana na mapendekezo ya UGTT kama mwanzo wa kutatua mgogoro wa kisiasa nchini," alisema Ghanouchi.

Maandamano ya kuipinga serikali ya Tunisia.
Maandamano ya kuipinga serikali ya Tunisia.Picha: Reuters

Naye katibu mkuu wa UGTT alithibitisha kuwa Ennahda ilikubaliana na mpango wa chama hicho kama msingi w akuanza majadiliano ya kitaifa na upinzani. Tunisia ilitumbukia katika mgogoro mpya wakisiasa kufuatia kuuawa kwa mwanasiasa wa upinzani Mohamed Brahmi, mgogoro wa pili wa aina hiyo katika kipindi cha miezi sita, na kusababisha maandamano mak,ubwa na miito ya kuitaka serikali ijiuzulu.

Mapendekezo ya UGTT
UGTT imependekeza kuundwa kwa serikali isiyoegemea vyama, wakati bunge likiendelea kuwepo na kuheshimu ratiba ya kuunda katiba mpya na kufanya uchaguzi mpya. Ghanouchi na Abbasi hawakusema iwapo Ennahda itakubali mabadiliko katika serikali, na hawakukubali kujibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari. "Ennahda imetoa mapendekezo kadhaa na tunakwenda kuyawasilisha kwa upande wa upinzani, kama yatakubaliwa, tutaanza mjadala wa kitaifa," alisema Abassi.

Katibu mkuu huyo wa UGGT alitarajiwa kukutana na wawakilishi wa kundi la upinzani, ambalo limekataa mara kwa mara kuzungumza na Ennahda, wakati muungano unaoongozwa na chama hicho bado uko madarakani, na badala yake ukitaka kuundwa kwa utawala mpya wa viongozi wa kujitegemea. Kwa upnade wake, Ennahda imekataa kushiriki mazungumzo ambayo masharti yake ni kuondoka kwa serikali, na badala yake ikapendekeza serikali ya umoja wa kitaifa, na kufanyika uchaguzi mpya mwezi Desemba.

UGTT ambayo inajivunia wanachama 500,000 na yenye uewezo wa kuikwamisha nchi, imekuwa na jukumu muhimu katika mazungumzo, ikizunguka kati ya vyama vinavyotawala na wapinzani katika jitihada za kutanzua mkwamo wa kisiasa. Muunagano wa National Salvation Front, ambao unavileta pamoja vyama vya upinzani, umeitisha maandamano ya nchi nzima, kuanzia Jumamosi jioni nje ya viwanja vya bunge.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle akiwa na rais wa Tunisia Moncef Marzouki, alipoitembelea Tunisia wiki iliyopita.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle akiwa na rais wa Tunisia Moncef Marzouki, alipoitembelea Tunisia wiki iliyopita.Picha: picture-alliance/dpa

Tuhuma za upinzani dhidi ya Ennahda
Wanahakarati na wabunge wa upinzani wamekuwa wakikusanyika hapo katika miezi iliyopita, kwa maandamano ya ya mara mbili, tarehe 6 na 13 Agosti, ambayo yalishirikisha maelfu ya waandamanaji. Ukiachilia mbali makabiliano ya hapa na pale mwishoni mwa mwezi wa Julai, maandamano hayo yamekuwa ya amani kwa ujumla, na waziri mkuu Ali Larayedh alionya dhidi ya kuzishambulia taasisi za serikali.

Upinzani unakituhumu chama cha Ennahda kwa kuharibu uchumi na kushindwa kuboresha viwango vya maisha. Shutuma hizo ni swa na zile zilizotolewa dhidi ya rais alieondolew anchini Misri na waandamanaji walioingia mitaani kabla ya jeshi kuingilia kati na kumn'goa madarakani tarehe 3 Julai.

Ennahda pia imetuhumiwa kwa kuwa walaini juu ya Waislamu wenye itikadi kali, ambao wanatuhumiwa kwa mauaji ya Brahmi na Chokri Belaid, mwanasiasa mwingine maarufu, ambaye kuuawa kwake kuliiangusha serikali ya kwanza iliyokuwa inaongozwa na Ennahda. Vyama vya Kiislamu vinautuhumu upinzani kw akujaribu kurudia yale yaliyotokea nchini Misri, ambako rais aliechaguliwa kidemokrasia aliondolewa katika mapinduzi yaliyofuatiwa na vurugu na kuwekwa kizuizini kwa vingozi wa Udugu wa Kiislamu.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/afpe
Mhariri: Mohamed Khelef