SiasaUturuki
Erdogan ashauri kuunda tume kuchunguza mkasa wa bwawa
7 Juni 2023Matangazo
Kiongozi huyo ametoa pendekezo hilo alipozungumza kwa njia ya simu kwa nyakati tofauti na Rais Vladimir Putin wa Urusi na Volodymyr Zelensky wa Ukraine.
Kwa mujibu wa ikulu ya Uturuki, Erdogan, ametanabahisha viongozi hao wawili kuwa uchunguzi huru na kina unahitajika ili kubaini ukweli wa kushambuliwa kwa bwawa la Kakhovka.
Erdogan ameshauri kwamba jopo la wachunguzi linaweza kuwajumuisha maafisa wa Umoja wa Mataifa na Uturuki.
Tangu kutokea mkasa huo hapo jana, Ukraine na Urusi zimeshutumiana kwa kila upande kuulaumu mwingine kuhusika na uharibifu wa bwawa hilo uliosababisha mafuriko yasiyo mfano kusini mwa Ukraine.