Erdogan azindua kanisa la kwanza kuliunga mkono
8 Oktoba 2023Matangazo
Ufunguzi wa kanisa hilo la madhehebu ya Orthodox unaashiria kipindi muhimu cha kitamaduni na kisiasa kwa Uturuki na kwa Erdogan mwenyewe, mwanasiasa mwenye nguvu anayejinasibisha na msimamo wa Kiislamu.Erdogan amekuwa akikosolewa vikali katika utawala wake wa miongo miwili kwa kubadili makanisa ya kale kuwa misikiti na kufanya uhafidhina wa Kiislamu kuwa na nguvu kubwa katika jamii.Kiongozi huyo aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa kanisa hilo la Wakristo wa kale wa jamii ya Wasuriya mjini Istanbul mnamo mwaka 2019. Wengi wa Wakristo hao wa asili wamehamia nchini humo tangu zama za kale wakitokea Syria na Iraq.