Ethiopia, Somaliland zakubaliana katika matumzi ya bandari
2 Januari 2024Kwa muda mrefu Ethiopia imekua ikiitegemea zaidi nchi jirani ya Djibouti, katika ufanyaji wa biashara zake zinazotegemea bandari.Akizungumza katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika mjini Addis Ababa, pamoja na Rais wa Somaliland Muse Bihi Abdi, Waziri Ahmed amesema, jambo hilo kwa sasa tayari limekubaliwa na jirani zao wa Somaliland na hati ya makubaliano imeshasainiwa. Rais Abdi kwa upande amesema, mojawapo ya makubaliano katika mkataba huo ni Ethiopia kuitambua Somaliland kama nchi na taifa huru linalojiongoza.Kwa mujibu wa Mshauri wa Usalama wa Taifa, Abiy Redwan Hussien, makubaliano hayo yamefungua njia kwa kuiruhusu Ethiopia kuendesha shughuli zake za baharini katika eneo hilo, nakuiwezeshakukifikia kituo cha kijeshi kilichokodishwa kwenye bahari ya Sham. Somaliland bado haijatambuliwa kimataifa licha ya kutangaza inajitawala tangu mwaka 1991, Somalia imekua ikiendelea kusema Somaliland ni sehemu ya eneo lake.