Ethiopia yawahamisha maelfu kutokana na kitisho cha volkano
4 Januari 2025Maelfu ya raia katika eneo la ndani la kaskazini mashariki mwa Ethiopia wamelazimika kuhamishwa kutokana na kitisho cha kutokea mlipuko wa volkano.
Zoezi hilo linafanyika baada ya mitikisiko kadhaa midogo kushuhudiwa tangu siku ya Alhamisi kutoka katika Mlima Dofen na kuzua hofu ya mlipuko kamili wa volkano ambayo inaweza kuweka watu wengi hatarini.
Soma: Mapigano mapya yaripotiwa katika jimbo la Afar, Ethiopia
Kulingana na idara ya usimamizi wa maafa katika mkoa wa Afar, tope la volkano linalotiririka kutoka mlima Dofen limesababisha nyufa kubwa kwenye miundombinu muhimu, ikiwemo barabara kuu na kuharibu mali.
Afar ni mojawapo ya maeneo kame na yenye joto zaidi nchini Ethiopia, yenye historia ya milipuko ya volkano na matetemeko ya ardhi ya mara kwa mara.