1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoQatar

Qatar: Eto'o aomba radhi kwa kuzozana na shabiki

7 Desemba 2022

Rais wa shirikisho la kandanda la Cameroon Samuel Eto'o ameomba radhi kwa kumpiga teke na kumwangusha mtu mmoja katika kile alichokiita ugomvi wa kurushiana maneno nje ya uwanja wa mechi za Kombe la Dunia.

https://p.dw.com/p/4KazJ
Fußball Smuel Eto'o
Picha: Omar Zoheiry/dpa/picture alliance

Rais wa shirikisho la kandanda la Cameroon na mchezaji nyota wa zamani Samuel Eto'o ameomba radhi kwa kumpiga teke na kumwangusha mtu mmoja katika kile alichokiita ugomvi wa kurushiana maneno nje ya uwanja wa mechi za Kombe la Dunia.

Eto'o alikuwa akipiga picha na mashabiki karibu na uwanja baada ya Brazil kuibwaga Korea Kusini 4 -1.

Video ilimuonyesha Eto'o akizuiwa na kundi la watu kabla ya kumrushia teke mwanaume huyo.

Eto'o amesema katika taarifa kuwa kulikuwa na ugomvi na shabiki huyo ambaye huenda alikuwa ni wa Algeria.

Ameomba radhi kwa kutojizuia na kufanya kitendo hicho ambacho hakiendani na hulka yake.