1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU: Makampuni yatakayosababisha athari za kijamii kuwajibika

14 Desemba 2023

Kamati ya bunge la Umoja wa Ulaya na nchi wanachama wa Umoja huo, zimekubaliana kuhusu sheria mpya zitakazofuatilia na kuyawajibisha makampuni makubwa yatakayosababisha athari mbaya za kijamii na kimazingira.

https://p.dw.com/p/4a8rU
Brüssel | Bunge la Umoja wa Ulaya likiwa katika vikao vyake vya kawaida
Bunge la Umoja wa Ulaya likiwa katika vikao vyakePicha: Dwi Anoraganingrum/Future Image/IMAGO

Haya yametangazwa leo katika chapisho la kamati hiyo kupitia mtandao wa kijamii wa X.

Chini ya makubaliano hayo yalioafikiwa leo asubuhi mjini Strasbourg, Ufaransa, makampuni ya ukubwa fulani katika Umoja wa Ulaya, yatahitajika kufuatilia na kushughulikia masuala kamaajira kwa watoto, utumwa, unyanyasaji wa wafanyakazi, uchafuzi wa mazingira, uharibifu wa mazingira na viumbe hai katika  hatua mbalimbali za mchakato wa uzalishaji bidhaa zao katika nchi mbali mbali.

Soma pia:Umoja wa Ulaya wakubaliana juu ya sheria muhimu ya AI

Sheria hizo mpya pia zitatumika kwa mashirika ya kimataifa yanayofanya biashara muhimu katika Umoja wa Ulaya.

Mara baada ya kupitishwa, Ujerumani inatarajiwa kuimarisha sheria zake zilizopo.

Makubaliano hayo bado yanapaswa kuthibitishwa na bunge la Ulayana matifa wanachama lakini huu ni utaratibu wa kawaida.