1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwanini EU imekataa kuisaidia Yemen

26 Aprili 2018

Mzozo wa Yemen ulianza mwaka 2011. Hata hivyo Umoja wa Ulaya unaonekana kuvitilia uzito zaidi vita vinavyoendelea nchini Syria, vilivyoanza wakati sawa.

https://p.dw.com/p/2wjur
Jemen Feuer in Lagerhalle in Hodeida
Picha: Reuters/A. Zeyad

kutokana na mazingatio ya kiuchumi pamoja na kutokuwepo na haraka kuhusu suala la wakimbizi.

Jumapili iliyopita, shambulio la angani lilipiga mahala palipokuwa na sherehe ya harusi nchini Yemen, ambapo vyanzo vya habari vinakadiria kuwa zaidi ya watu 20 waliuawa na wengini 50 kujeruhiwa.

Mashambulizi hayo yalilaumiwa kwa Saudia Arabia, ambayo serikali yake inalenga kushinda waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.

Saudi Arabia yalaumiwa

Ijapokuwa mashambulio ya angani katika maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi yamesababisha vifo vya raia mara kwa mara katika kipindi cha miaka saba ya mzozo wa Yemen –mataifa ya Umoja wa Ulaya — yakiwemo Ufaransa na Uingereza, yamefanya kidogo kuyalaani mashambulio hayo wala kuingilia kati mzozo huo.

Günter Meyer, mkurugenzi wa kituo cha Utafiti kuhusu mataifa ya Kiarabu katika Chuo Kikuu cha Mainz, ameiambia Deutche Welle, "Mataifa ya Uingereza na Ufaransa yanaiuzia silaha Saudi Arabia, kumaanisha kuwa hawaoni haja ya kujishughulisha na janga la kibinadamu katika eneo hilo."

Jemen Krieg | Aden, Kämpfe
Mlipuko katika mji wa Bandari ya AdenPicha: Reuters/F. Salman

Meyer anaongeza kusema kuwa mataifa ya Umoja wa Ulaya hayana sababu za msingi za kusaidia kwenye mzozo wa Yemeni, lakini sababu za kiuchumi na kisiasa na Saudi Arabia zinapewa uzito kwanza.

Ali al-Absi, mtafiti aliyejikita katika masuala ya Umoja wa Ulaya na mshauri katika Baraza la Bishara na Viwanda la mataifa ya Kiarabu na Ujerumani ameiambia Deutche Welle,  "mataifa ya Umoja wa Ulaya pia hayajaridhishwa na serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia na kwa hivyo yana wasiwasi juu ya kuusadia utawala wa Yemen kifedha."

Kuna madai kuwa maafisa wa serikali ya Yemen kuwa wafisadi. Mbali na hayo, anasema kuwa huenda Umoja wa Ulaya unaona Saudi Arabia na Falme za Kiarabu kuwa matajiri ambao wanaweza kulisaidia taifa la Yemen bila ya kulihusisha taifa lingine.

Kile ambacho kinawashangaza wadadisi wengi sio kutoingilia kwao, lakini ni hatua yao ya kutolaani uvamizi huo.

Hiyo ni kwasababu mataifa ya Umoja wa Ulaya kama vile Uingereza na Ufaransa yana mahusiano ya karibu na Saudi Arabia, yanafanya biashara ya silaha pamoja na mambo mengine ya kibiashara, hivyo yananyamaza raia wakiuliwa kwenye mashambulio ya angani ambapo takribani watu elfu 10 wameuawa tangu kuzuka kwa mzozo wa Yemen.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mwezi Aprili mwaka 2016, zaidi ya asilimia 60 ya vifo nchini Yemen vilisababishwa na mashambulio ya angani yaliyotekelezwa na Saudia Arabia.

EU haijalaani mashambulio dhidi ya Yemen

Ufaransa na Uingereza yana mahusiano ya karibu na mwanamfalme Mohammed bin Salman, ambaye kimsingi ndiyo mwenye maamuzi muhimu katika ufalme huo. Kwa mujibu wa Reuters, wakandarasi wa jeshi la ulinzi la Ufaransa waliuza silaha za thamani ya euro bilioni mbili kwa Saudi Arabia mwaka 2015.

Takwimu zilozochapishwa na idara ya biashara ya Uingereza mwezi Oktoba zilionyesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017 mauzo ya silaha kutoka Uingereza hadi Saudi Arabia yalifikia euro bilioni 1.25

Mama anajitahidi kumlisha mwanaye
Mama anajitahidi kulisha mwanayePicha: DW/J. Abdullah

Mashirika ya kutetea haki za binadamu kama vile Amnesty International yamekosoa biashara hiyo ya silaha.

Ghorfa's al-Absi anasema, "sababu moja ambayo huenda ikachangia serikali ya kansela Angela Merkel kusitisha mauzo ya silaha kwa Saudia Arabia ni kwa kuwa sekta ya silaha siyo muhimu sana kwa pato la jumla la taifa la Ujerumani kama ilivyo kwa Ufaransa na Uingereza."

Wakimbizi ni sababu nyingine ambayo mataifa ya Umoja wa Ulaya yamevutiwa kuingilia kati vita vya Syria huku yakipuuza Yemen. Watu wapatao milioni moja kati ya Wasyria milioni 11 waliopoteza makaazi yao na wametafuta hifadhi mataifa ya Umoja wa Ulaya. Hali ni tofauti nchini Yemen, anasema al-Absi.

Badala ya kujaribu kuja barani Ulaya kama wakimbizi kupitia njia ngumu ambayo ingewalaazimisha kupitia Saudi Arabia na yumkini Syria, Iraq au zote, watu waliopoteza makaazi yao huko wanakimbilia katika maeneo salama yaliosalia nchini humo.

Karibu watu milioni tatu wamekuwa wakimbizi wa ndani Yemen, na hadi pale watakapojaribu kufanza safari hatari kwenda Ulaya, Umoja wa Ulaya, utakuwa na maslahi kidogo katika mgogoro huo kuliko ulivyo na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, anasema al-Absi.

Lakini rais Bashar Assad anavyozidi kuteka maeneo mengi yaliyokuwa yanakaliwa na waasi nchini Syria, viongozi wa Umoja wa Ulaya huenda wakachelewa kulipa uzito janga la kibanadamu nchini Yemen.

Mwandishi: Shisia Wasilwa, Dw

Mahriri: Iddi Ssesenga