EU yaongeza watu tisa katika orodha yake ya vikwazo
26 Julai 2024Matangazo
Hatua hiyo inawalenga makamanda kadhaa wa makundi kadhaa na muungano unaoitwa Muungano wa Mto Kongo, na kufanya hesabu jumla ya walioingia kwenye orodha ya vikwazo vyake kwa ajili ya Kongo kufikia 31.
UN yawawekea vikwazo waasi wa Kongo huku mapigano yakiendelea
Katika taarifa, Baraza la Umoja wa Ulaya limesema kuwa walioorodheshwa walishutumiwa kwa vitendo vinavyojumuisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na kwa kuendeleza migogoro ya silaha, ukosefu wa utulivu na usalama Mashariki mwa nchi hiyo.
Kuorodheshwa kwa Muungano wa Mto Kongo unaojulikana kwa jina la Kifaransa kama Alliance Fleuve Congo", ama AFC, kunakuja siku moja baada ya Marekani pia kuuwekea vikwazo muungano huo.