EU: Yapendekeza pasi maalum ya chanjo ya virusi vya corona
1 Machi 2021Matangazo
Von der Leyen amesema katika ujumbe wa Twitter kuwa pasi hiyo ya kidigitali ya kijani, italenga kutoa uthibitisho wa kuchanjwa na matokeo ya vipimo vya covid-19.
Pasi hiyo itawaruhusu watu kutembea kwa usalama katika nchi za Umoja wa Ulaya au nje kwa ajili ya kazi au utalii.
Katika mkutano mwingine na wabunge wa Ujerumani katika bunge la shirikisho na wale wa Bunge la Ulaya, von der Leyen amesema Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya itaanzisha cheti maalum cha kidijitali katika miezi ijayo kitakachokubalika na nchi 27 wanachama wa umoja huo.