1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yatangaza msaada mpya wa kiutu kwa Waukraine

13 Januari 2025

Umoja wa Ulaya umetangaza msaada mpya Euro milioni 140 kwa Ukraine na Euro zingine milioni 8 zaidi kutoka Moldova. Msaada huo unalenga kwenda kuwasaidia watu walioathirika na vita vinavyoendelea.

https://p.dw.com/p/4p7mk
Ukraine | Rais Volodymyr Zelensky
Rais Volodymyr Zelensky Picha: John Thys/AFP

Msaada huo ulitangazwa wakati Kamishna wa Umoja huo Hadja Lahbib, anayehusika na usimamizi wa migogoro, alipotembelea Ukraine ili kujadili changamoto zinazowakumba binadamu kwenye vita vya nchi hiyo na Urusi vinavyoendelea. Lahbib amesema msaada huo unalenga kuwasaidia Waukraine wapate chakula, makazi,maji safi na umeme.

Wakati huo huo mashambulizi kati ya Ukraine na Urusi yameendelea kuripotiwa hii leo. Urusi imeishutumu Ukraine kwa kufanya mashambulizi ya droni kwenye miundombinu ya bomba kubwa la gesi ambalo husafirisha gesi kutoka Urusi kwenda Ulaya kupitia Uturuki.

Soma pia:Austin amrai Trump kutoyatupa mapambano ya Ukraine dhidi ya Urusi

Mapema leo, Ukraine nayo iliripoti kuzidungua droni 78 kati ya 110 zilizorushwa na Urusi usiku wa kuamkia leo Jumatatu.