EU: Yaweka vikwazo kwa utawala wa kijeshi Niger
23 Oktoba 2023Matangazo
Umoja huo wenye wanachama 27 aidha umeilaani hatua ya kumuondoa rais aliyechaguliwa kidemokrasia, Mohamed Bazoum, ambaye ni mshirika mkubwa wa mataifa ya Magharibi.
Umoja wa Ulaya umetangaza kupitisha mfumo wa kisheria ambao utauwezesha kuwawekea vikwazo watu binafsi na vyombo vinavyohusika na vitendo vinavyotishia amani, utulivu na usalama wa Niger.
Soma pia:Kiongozi wa zamani wa Niger pamoja na familia yake wanaendelea vizuri
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja huo, Joseph Borrell, amesema hatua hiyo inatuma ujumbe wa wazi kwamba mapinduzi ya kijeshihuwa na gharama.