1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

F1: Hamilton ashinda mashindano ya Italia

3 Septemba 2018

Bingwa wa ulimwengu wa mashindano ya magari ya Formula One Lewis Hamilton ameifikia rekodi ya Michael Schumacher ya kushinda mara tano mashindano ya Grand Prix nchini Italia.

https://p.dw.com/p/34Dop
Italien Grandprix Formel 1 Monza
Picha: Reuters/S. Rellandini

Ushindi wa Hamilton wa timu ya Mercedes uliacha timu ya Ferrari ikiwa na uchungu kwa mara nyingine katika ngome yao ya nyumbani. Muingereza Hamilton na Mjerumani Sebastian Vettel, mpinzani wake wa karibu ambaye anafuata nyuma na pengo la pointi 30, waligogangana katika mzunguko wa kwanza na Vettel akajikuta katika nafasi ya 18 kabla ya kupambana na kumaliza katika nafasi ya nne.

Hamilton kisha akampiku Kimi Raikkonen mara mbili, ambaye alikuwa ameanza mashindano hayo katika nafasi ya kwanza na kuivunja mioyo ya mashabiki wa Ferrari ambao walitaka kusherehekea ushindi wa kwanza katika ardhi ya nyumbani katika miaka minane. Huyu hapa Hamilton "kwanza nataka kuwapongeza Ferrari kwa kutupa ushindani mkali wikendi hii. Walifanya kazi nzuri sana na wanaonyesha mapambano makali. Pili, nataka tu kuwashukuru mashabiki wote hapa na walioko nyumbani, kwa sababu bila ya uungaji wao mkono, bila ya juhudi zao za kila siku hili halingewezakana leo" Alisema Modric.

Ushindi huo wa sita wa Hamilton msimu huu umeongeza pointi zake kilele hadi 256, dhidi ya Vettel ambaye ana 226. Kuna mashindano saba yaliyobaki msimu huu. Dereva wa Mercedes Valtteri Bottas alimaliza katika nafasi ya tatu.

Na sasa tumalizie Afrika ambapo, Mashindano ya kimataifa ya Afrika ya karate yamefikia kilele chake jana jijini Kigali Rwanda. Mabingwa Misri ndiyo waliibuka kidedea barani Afrika wakijizolea medali nyingi za dhahabu. Afrika mashariki iliwakilishwa na nchi mbili ambazo ni Kenya na Rwanda, mwenyeji wa mashindano hayo. Mwandishi wetu Christopher Karenzi anasimulia zaidi

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Mohammed Khelef