1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA: Ujerumani bado ni timu bora

Sekione Kitojo
16 Oktoba 2017

Ujerumani imeendelea kukalia nafasi ya juu ya orodha ya timu bora duniani  kwa  sasa iliyotolewa  na shirikisho la kandanda duniani FIFA kama ilivyochapishwa Jumatatu na kuthibitisha timu za kiwango cha  juu.

https://p.dw.com/p/2lvi8
Fußball WM 2018 Qualifikation Deutschland vs Nordirland
Picha: picture alliance/dpa/GES/M. I. Güngör

Timu hizo zitakazowekwa  katika chungu  kimoja  katika  upangaji  wa timu zitakazoshiriki  katika makundi  ya  fainali  za  kombe  la  dunia mwakani , pamoja  na michuano  ya  mchujo  ya  kombe  la  mataifa  ya  bara  la  Ulaya.

Mabingwa  wa  dunia  Ujerumani , Brazil , Ureno , Argentina, Ubelgiji , Poland  na  Ufaransa  zinajiunga  na  Urusi  kuwa  timu zitakazowekwa  katika  chungu cha  kwanza katika  upangaji  wa timu  hapo Desemba  mosi kwa  ajili  ya  fainali  za  mwaka  2018.

Deutschland Joachim Löw in Mainz
Timu ya taifa ya Ujerumani ikifanya mazoweziPicha: picture alliance/GES/M. Gilliar

Katika upangaji  wa  makundi  kwa  ajili  ya  michuano  ya  kufuzu kucheza  katika  fainali za  kombe  la  mataifa  ya  Ulaya  hapo kesho  Jumanne, Uswisi, Italia, Croatia  na  Denmark  zitakuwa miongoni  mwa  timu  za  juu, wakati  Ireland ya  kaskazini , Sweden , Ireland  na  Ugiriki ni  timu za  chungu  cha  pili.

Timu bora 6 hazijabadilika

Katika  orodha  ya  FIFA  ya  timu  bora , timu  6  za  juu hazijabadilika, wakati  Ufaransa imepanda  nafasi  moja  hadi  ya saba na  Uhispania  imepanda  nafasi  tatu  hadi  nafasi  ya  nane lakini  hazimo  katika chungu namba  moja.

Chile, ambayo  imeshindwa  kufuzu  kucheza  katika  fainali  za kombe  la  dunia , imebakia  kiuwa  katika  nafasi  ya  tisa wakati Peru  imeingia  katika  kumi  bora kwa  mara  ya  kwanza, ikipanda nafasi  mbili hadi  ya  kumi. Peru imefanikiwa  kuingia  katika  mchezo wa  mchujo wa mabara  dhidi  ya  New Zealand ikiwa  katika  nafasi ya  122  katika  juhudi  zao  za  kufikia  fainali  za  kombe  la  dunia.

Kwingineko Uingereza  imepanda  nafasi  tatu  hadi  12 wakati timu nyingine  zilizopiga  hatua  ni pamoja  na  Denmark  iliyopanda  nafasi saba  hadi  ya  19, Scotland  ikiwa   katika  nafasi ya 29, Austria , 39. Wenyeji  wa  kombe  la  dunia  Urusi  iko  katika  nafasi  ya  65.

Tunesien Tunis Afrobasket 2017 Gewinner Tunesien
Picha: picture-alliance/Zumapress/C. Mahjoub

Kwa upande  wa  Afrika  Tunisia inaongoza  bara  hilo nafasi iliyoshika  miaka  15 iliyopita  kwa kukaribia  kufuzu  kucheza  katika fainali  za  kombe  la  dunia  mwakani. Ushindi  wa  mabao 4-1 dhidi ya  Guinea  wa Tai wa Carthage ni  mafanikio  makubwa  kwa  kocha Nabil Maaloul. Misri iliyokata tikiti  yake katika  fainali  za  kombe  la dunia  kwa  kuishinda  Congo  Brazzaville mwishoni  mwa  juma lililopita , imeporomoka nafasi  moja na  kushika nafasi  ya  pili wakati  Morocco  imepanda  nafasi  tatu na  kushika  nafasi  ya saba.  Senegal  ni  ya  tatu, (32)ikifuantiwa  na  jamhuri  ya kidemokrasi  ya  Congo,(35) , Nigeria ni  ya  tano (41), Cameroon ni ya  6, (42), Morocco  ya 7, (48), Ghana  ni  ya  nane (52), Burkina Faso ni  ya  9 , (55) na  Cote d'ivoire ni  ya 10 (61).

 

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre / dpae / ape

Mhariri: Mohammed  Abdul-Rahman