1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA yaandaa mkutano mkuu Mexico

13 Mei 2016

Rais mpya wa FIFA Gianni Infantino ameongoza mkutano mkuu wa kandanda la dunia wa kila mwaka ulioandaliwa jana mjini Mexico City ambao ulidhamiria kuyapa msukumo mageuzi mapya

https://p.dw.com/p/1IncT
FIFA Präsident Gianni Infantino
Picha: picture-alliance/dpa/R. Sitdikov

Mageuzi hayo yanalenga kuirekebisha taswira ya shirikisho hilo lililochafuliwa na kashfa za rushwa.

Infantino alisema anataka kuufungua ukurasa mpya kwa ajili ya kuliboresha kandanda "Kama mnavyojua FIFA imepitia wakati mgumu sana. Ninatoa shukrani mbele yenu nyote, kwa Rais Issa Hayatou kwa kuliokoa jahazi hili. Kwa miezi kadhaa, rais wa FIFA na mkutano mkuu wa FIFA walipitisha mageuzi muhimu ambayo yataleta uwazi na uongozi bora na hilo limefaulu kutokana na misingi ya kazi. Nikiwa Rais wa FIFA, nitaendeleza kazi hii pamoja nanyi nyote katika mashirikisho ya wanachama wa bara la Afrika

FIFA sasa lazima iidhinishe mageuzi yaliyopitishwa katika mkutano mkuu maalum mwezi Februari, ambao ulilibadilisha jina la kamati kuu ya FIFA kuwa Baraza la FIFA na kupunguza mamlaka yake.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef