FIFA yapitisha mageuzi makubwa ya soka
26 Februari 2016Wajumbe 207 toka 209 wanachama wa taasisi hiyo ya kimataifa wameshiriki katika kumchagua mtu atakayeshika nafasi ya Sepp Blatter aliyesitishwa wadhifa wake kutokana na madai ya rushwa.
Wagombea 4 ndio waliokuwa wamesalia baada ya Tokyo Sekwale wa Afrika Kusini kujitoa. Gianni Infantino wa Uswsisi ameibuka na kura 88 katika duru ya kwanza akifuatiwa na Sheikh Salman kwa kura 85.Mgombea alihitaji kura 138 kuibuka na ushindsi katika duru ya kwanza.Duru ya pili inaendelea.
Kabla ya hapo wajumbe waliunga mkono kwa sauti 179 dhidi ya 22 kuunga mkono hatua zinazopunguza hadi mihula mitatu badala ya mihula minne,muda wa viongozi kuendesha nyadhifa zao. Wameunga mkono pia shauri la viongozi kuacha wazi mapato yao.
Taasisi mpya ya uongozi wa FIFA itakuwa na jukumu la kusimamia masuala yote ya fedha yanayolihusu shirikisho hilo la kimataifa.
Baraza lenye wanachama 36,wakiwemo angalao wanawake sita,watakaochaguliwa na mashirika ya soka ya kitaifa, litajishughulisha kwa upande wake na masuala ya kisiasa na kimkakati.
Taasisi hizo mbili zitasimamiwa na halmashauri maalum ya kuchunguza hesabu na kuhakikisha kama zinalingana.
Mwenyekiti wa tume ya marekebisho Francois Carrard amewasilisha mswaada wa kurasa 62 akiwaeleza wajumbe mkutanoni wanabidi waituimie fursa pekee iliyojitokeza kuleta mageuzi katika utendaji wa taasisi hiyo.
"Mageuzi haya ni muhimu ili kulazimisha mageuzi ya kina katika desturi za FIFA. Demokrasia itakuwa kubwa zaidi,utawala utakuwa bora zaidi kutokana na kugawanywa madaraka,kutakuwa na hali kubwa zaidi ya uwazi na wanawake watakuwa wengi zaidi". "Mpango huu wa mageuzi utamwezesha mwenyekiti mpya na auongozi mpya kujenga msingi wa hali ya siku za mbele."Amesema mwenyekiti wa tume ya marekebisho Francois Carrard.
Mwandishi: Hamidou Oummilkheir/dpa/afp
Mhariri: Josephat Charo