Finland kuwazuia watafuta hifadhi kuingia nchini humo
21 Mei 2024Mpaka huo mara kwa mara hufunikwa na theluji na Finland inaamini serikali ya mjini Moscow inaunga mkono kutokana na upinzani wa kisiasa tangu kuzuka vita vya Ukraine.
Waziri Mkuu wa Finland Petteri Orpo ameuambia mkutano wa waandishi habari kwamba ni jukumu la serikali kuhakikisha usalama wa mipaka, taifa la Finland na raia wa Finland katika hali zote.
Orpo pia amesema kwa bahati mbaya sheria ya Umoja wa Ulaya haiwapi nyenzo madhubuti kulitatua tatizo hilo, akitumai kwamba kazi yao itafungua mlango kwa kupatikana suluhisho katika ngazi ya Umoja wa Ulaya.
Finland iliufunga mpaka wake wa kilometa 1,340 kufuatia ongezeko la wahamiaji waliowasili kutoka nchi kama vile Syria na Somalia muda mfupi baada ya Finland kujiunga na jumuiya ya kujihami ya NATO.