1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Frankfurt na Augsburg zatoka sare

21 Desemba 2013

Bundesliga ambapo Eintracht Frankfurt wameikamilisha nusu ya kwanza ya msimu bila kupata ushindi hata mmoja katika michezo ya nyumbani, baada ya kutoka sare ya kufungana goli moja kwa moja na Augsburg Ijumaa

https://p.dw.com/p/1AeVr
Fußball Bundesliga Eintracht Frankfurt gegen FC Augsburg
Picha: picture alliance/dpa

Raul Robadilla alitikisa nyavu na kuwaamusha mashabiki wa Augsburg katika dakika ya 33 lakini Jan Rosenthal akawasawazishia wenyeji Frankfurt dakika tatz kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika. Kocha wa Frankfurt Armin Veh, katika mchuano wake wa 250 wa Bundesliga, alikuwa na kila sababu ya kumshukuru mlinda lango Kevin Trapp kwa kuwapa matokeo hayo wakati alipolizuia kombora lililofyatuliwa na Arkadiuz Milik wa Augsburg ambaye alikuwa amebaki yeye peke yake na mlinda lango wakati zikiwa zimesalia dakika tano mechi kumalizika.

Katika mechi zinazoendelea kwa sasa, timu inayoshikilia nafasi ya pili katika ligi Bayer Leverkusen inapambana ugenini na Werder Bremen, wakati ile inayoshikilia nafasi ya tatu Borussia Dortmund, ikiwa nyumbani na Hertha Berlin. Nuremberg wanawaalika Schalke 04 wakiendeela kutafuta ushindi wao wa kwanza kabisa msimu huu. reiburg wako nyumbani na Hanover 96, wakati Hamburg ikimenyana na Mainz 05. Eintracht Braunschweig inafunga kazi na Hoffenheim. Borussia Moenchengladbach watakuwa wenyeji wa VfL Wolfsburg kesho Jumapili.

bu ya Raja Casablanca ya Morocco inataraji kutimiza ndoto yao leo kwa katika fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu, kwa kuwabwaga mabingwa wa Ulaya Bayern Munich.

Taifa zima lizakuwa nyuma ya Raja Casablanca lakini pia Bayern ina wapenzi wake
Taifa zima lizakuwa nyuma ya Raja Casablanca lakini pia Bayern ina wapenzi wakePicha: DW/ A. Errimi

Klabu hiyo iliiduwaza Atletico Mineiro ya Brazil katika nusu fainali kwa kuirambisha magoli matatu kwa moja. Mabingwa hao wa Morocco ambao walifuzu tu, kwa ajili ya kuwa wao walikuwa wenyeji wa dimba hilo, wamechinda mechi zite tatu kuelekea katika fainali.

Waliwashinda Auckland City magoli mawili kwa moja, na kisha wakawazidi nguvu CF Monterrey wa Mexico kwa matokeo sawa na hayo. Waliwaangusha Mineiro wakiongozwa na Ronaldinho na kuwa timu ya pili kutoka Afriak kufika fainali ya Kombe la DUnia la Vilabu.

Nao Bayern walipata ushindi rahisi wa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Guangzhou Evergrande katika nusu fainali ya kwanza, na wako tayari kuufunga mwaka kwa kunyakua taji la tano.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP

Mhariri: Mohammed Dahman