1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FREIBURG: Dalai Lama amekamilisha ziara ya Ujerumani

29 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeD

Dalai Lama ameikamilisha ziara yake ya siku tisa nchini Ujerumani kwa kuikosoa China kuhusika na suala la haki za binadamu.Kiongozi huyo wa Ubudha wa Tibet amesema,wakati ambapo uchumi unafumuka nchini China,hakuna maendeleo yanayofanywa katika nchi hiyo kuhusu haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari na dini.Dalai Lama mwenye miaka 72,alitamka hayo kwenye karamu iliyofanywa katika makao makuu ya Halmashauri ya Jiji la Freiburg,kusini-magharibi ya Ujerumani.Mpokea Tuzo ya Amani ya Nobel,Dalai Lama alitoa wito kwa Ujerumani kutumia nguvu za ushawishi wake wa kiuchumi kwa China ili kusaidia kuhimiza mageuzi.