FREIBURG: Mgomo katika hospitali za vyuo vikuu
5 Oktoba 2005
Kwa mara ya mwanzo katika historia ya Ujerumani watumishi wa hospitali za vyuo vikuu wamegoma kufanya kazi kwa muda usiojulikana.Wauguzi, viongozi,mafundi na wapishi katika hospitali za miji ya Freiburg,Heidelberg,Tübingen na Ulm wanaupinga mpango wa kutaka kuongezewa muda wa kufanya kazi na kupunguziwa mishahara yao.Kwa mujibu wa jumuiya ya wafanyakazi -Verdi,huduma za dharura hazitoathirika wakati wa mgomo huo.Mwezi wa Septemba,mazungumzo kuhusu mishahara ya watumishi 25,000 wa hospitali zilizohusika yalishindwa kupata maafikiano.Kwa upande mwingine katika kiwanda cha AEG mjini Nuremberg wafanyakazi wana mgomo wa saa 24.Sababu ya kugoma kazi ni tangazo lililotolewa kuwa kiwanda hicho kitahamishwa Poland ili kupunguza gharama zake.Hatua hiyo itawaathiri wafanyakazi 1,750.