1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

G7 inapanga juhudi mpya za chanjo kwenye nchi zinazoendelea

13 Mei 2023

Kundi la nchi saba zilizoendelea zaidi kiuchumi duniani, G7 linatarajiwa kukubaliana kuhusu kuanzisha mpango mpya wa kusambaza chanjo kwenye nchi zinazoendelea katika mkutano wa kilele wa viongozi wa G7 wiki ijayo.

https://p.dw.com/p/4RIo8
Japan | Treffen der G7 Finanzminister
Picha: Kiyoshi Ota/Pool/REUTERS

Gazeti la Japan, Yomiuri limeripoti Jumamosi kuwa mpango huo mpya unakusudia kukusanya fedha kwa ajili ya kutengeneza na kununua chanjo, pamoja na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya, ili kujiandaa kwa janga lijalo la kimataifa.

Katika mkutano wa Jumamosi wa mawaziri wa fedha na mawaziri wa afya wa G7, wamekubaliana kutoa msaada kwa nchi zenye kipato cha chini na cha kati ili kusaidia kuongeza jukumu lao katika mfumo wa kusambaza bidhaa zinazohusiana na nishati.

Viongozi wa G7 watazingatia iwapo watoe tamko kuhusu jinsi ya kukabiliana na janga la kimataifa katika mkutano huo utakaofanyika kuanzia Mei 19 hadi 21, Hiroshima, Japan.