1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

G7 kutangaza mpango wa muda mrefu wa usalama kwa Ukraine

12 Julai 2023

Viongozi wa kundi la mataifa tajiri duniani, G7, watatangaza dhamira yao ya kuendelea kuisadiia Ukraine bila ukomo kwa kuimarisha jeshi la nchi hiyo na kuipatia uwezo wa kukabiliana na hujuma za miaka inayokuja

https://p.dw.com/p/4TlL1
Litauen | Nato-Gipfel in Vilnius | Treffen Wolodymyr Selenskyj und Olaf Scholz
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Tangazo hilo litatolewa pembezoni mwa mkutano wa NATO unaofanyika nchini Lithuania baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa kundi la G7 na Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.

Duru zinasema kundi la G7 litaweka mezani mpango mpana wa kuipatia Ukraine silaha za kisasa za kivita, mafunzo kwa wanajeshi wake na kubadilishana taarifa za kiintelinjesia pamoja na ulinzi wa mifumo ya mawasiliano ya mtandao.

Kundi hilo linalojumuisha mataifa ya Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Japan, Canada na Italia linalenga kutumia mpango huo kutuma ujumbe mzito kwa utawala wa Urusi kwamba kamwe hawataitupa mkono serikali mjini Kyiv.