Gabon, Guinea ya Ikweta zachuana mbele ya ICJ
1 Oktoba 2024Matangazo
Mnamo Jumatatu (Septemba 30), Guinea ya Ikweta ilitowalea wito majaji wa mahakama hiyo ya ICJ kuyakataa madai ya Gabon inayoshikilia kwamba visiwa hivyo ni vyake.
Nchi hizo mbili jirani ambazo zote zina utajiri wa mafuta zimeitaka mahakama hiyo ya kimataifa kusuluhisha mgogoro unaokihusisha kisiwa cha Mbanie kilichoko chini ya kilomita moja kutoka pwani ya Gabon.
Soma zaidi: Guinea ya Ikweta yaiomba ICJ kuyakataa madai ya Gabon
Mvutano huo umekuwa ukiendelea tangu mwaka 1972 baada ya jeshi la Gabon kuwaondowa wanajeshi wa Guinea ya Ikweta katika kisiwa hicho cha Mbanie.
Kesi hiyo iliyoanza inatazamiwa kusikilizwa kwa wiki nzima na uamuzi wa ICJ unatarajiwa kutolewa mwaka ujao.