Gabon kufanya uchaguzi wa rais mwezi Aprili
23 Januari 2025Matangazo
Msemaji wa serikali ya Gabon Serapin Akure Davain ametoa tangazo hilo mapema hii leo baada ya mkutano wa baraza la mawaziri.
Soma pia: Raia wa Gabon wapiga kura ya maoni kuhusu katiba mpya
Taifa hilo la Afrika lenye utajiri wa mafuta ambalo limetawaliwa na familia ya Bongo kwa miaka 55, ilipitisha katiba mpya katika kura ya maoni ya mwezi Novemba.
Rais wa mpito Jenerali Brice Oligui Nguema, aliyechukua wadhifa huo mara baada ya mapinduzi ya Agosti 2023, ameweka wazi azma yake ya kusalia madarakani.