SiasaGabon
Gabon yasimamishwa uanachama katika Umoja wa Afrika
1 Septemba 2023Matangazo
Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika, limesema jana jioni kwamba linalaani vikali unyakuzi wa madaraka uliofanywa na jeshi na kupinduliwa kwa Rais Ali Bongo.
Baraza hilo limetangaza kuisimamisha Gabon mara moja katika ushiriki wa shughuli zote ndani ya Umoja wa Afrika na taasisi zake hadi pale utaratibu wa kikatiba utakaporejeshwa nchini humo.
Wiki chache zilizopita Umoja wa Afrika ulisimamisha uanachama wa Niger baada ya jeshi kuchukua mamlaka mwishoni mwa mwezi Julai. Burkina Faso, Mali, Guinea na Sudan pia zimesimamishwa tangu kulipotokea mapinduzi katika nchi hizo.
Wakati huo huo duru zinasema Jenerali aliyeongoza mapinduzi Brice Oligui Nguema ambaye ni ndugu wa Rais Bongo ataapishwa siku ya Jumatatu kama rais wa mpito.