Gambia yagundua uwepo wa homa ya mafua ya ndege
6 Aprili 2023Matangazo
Mamlaka nchini Gambia zimegundua uwepo wa homa ya mafua ya ndege aina ya H5N1 kwa ndege wa mwituni aliye kwenye hifadhi, wiki moja baada ya nchi jirani ya Senegal kutangaza mripuko wa homa hiyo kwa wafugaji wa kuku.CAIRO: Msichana amefariki Misri kwa virusi vya H5N1
Sampuli za ugonjwa huo zilikusanywa kutoka Hifadhi ya Ndege ya Tanji nchini Gambia, karibu kilomita 20 kutoka mji mkuu Banjul na kutumwa katika maabara huko Dakar nchini Senegal baada ndege kadhaa wa mwituni kuripotiwa kufariki katika eneo hilo.
Mamlaka za Gambia zimesema zinashughulikia kwa karibu suala hilo ili kusaidia kupunguza shinikizo la maambukizi ya homa hiyo ya mafua ya ndege.