1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gavana wa Punjab auawa Pakistan

P.Martin/ZPR5 Januari 2011

Gavana wa jimbo la Punjab ameuawa baada ya kupigwa risasi na mlinzi wake katika mji mkuu wa Pakistan,Islamabad.

https://p.dw.com/p/QndG
Salman Taseer, governor of Pakistan's Punjab who was assassinated 4 January 2010 Tuesday. Foto: DW/Tanvir Shahzad
Gavana Salman Taseer wa jimbo la Punjab alieuawa.Picha: DW

Kwa mujibu wa maafisa wa polisi, watu wengine watano pia walijeruhiwa katika shambulio hilo.

Gavana Salman Taseer, ni mhanga mashuhuri kabisa kuuawa katika mashambulio yaliyofululiza nchini Pakistan, tangu waziri mkuu wa zamani Benazir Bhutto kuuawa katika mwaka 2007.

Taseer, alikuwa mshirika wa Rais Asif Ali Zardari,ambae ni mjane wa Bhutto. Hivi karibuni, gavana huyo aliikosoa sheria inayohusika na adhabu ya kutolewa kwa vitendo vya kufuru. Waislamu wenye itikadi kali wameitetea sheria hiyo.