Gaza. Majeshi ya Israel yaua wanne Palestina.
31 Oktoba 2007Matangazo
Shambulio la ndege za kijeshi la Israel limesababisha vifo vya Wapalestina wanne na kuwajeruhi wengine kadha katika eneo la kusini la ukanda wa Gaza. Watu walioshuhudia wamesema kuwa watu wanne waliouwawa walikuwa polisi wa chama cha Hamas. Jeshi la Israel limedhibitisha kuwa majeshi yake yamefanya shambulio hilo katika eneo la kijiji mashariki ya Khan Younis.
Msemaji wa jeshi hilo amesema shambulio hilo lililenga kile alichokieleza kuwa ni maeneo ya magaidi wa Hamas na limefanywa kujibu shambulio la maroketi dhidi ya eneo la Israel.