1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza, Palestina. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani awataka wapalestina kufanya juhudi zaidi kuimarisha amani.

23 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CErV

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesifu juhudi za Wapalestina za kuhakikisha usalama kabla ya zoezi la kujiondoa kwa Israel kutoka Gaza.

Lakini katika mazungumzo yake na viongozi wa Palestina , ikwa ni pamoja na rais Mahmoud Abbas katika eneo la ukingo wa magharibi, amesema kuwa wanapaswa kufanya juhudi zaidi.

Rice pia amerudia kuwa Marekani inaheshimu ahadi zake za kuhakikisha kuwa Israel inasitisha kabisa ujenzi wa makaazi mapya ya Wayahudi katika ardhi ya Wapalestina.