1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Blair akutana na wakuu wa Palestina

25 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfc

Mjumbe maalum wa pande nne zinazosaka amani Mashariki ya Kati, Tony Blair amekutana na viongozi wa mamlaka ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi ikiwa ni ziara yake ya kwanza toka alipoteuliwa.

Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Uingereza amesema kuwa ziara yake ya siku mbili katika eneo hilo ilikuwa ni nafasi ya kusikiliza, kujifunza na kuelezea yanayowezekana kufikia malengo.

Blair alikuwa na mazungumzo na Rais wa Palestina Mahamoud Abbas na Waziri Mkuu Salam Fayyad.Alitarajiwa pia kukutana na Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert.