GAZA:Mapambano kati ya wanajeshi wa Israel na wanamgambo wa Palestina
30 Juni 2005Matangazo
Taarifa zinaeleza kuwa ndege ya Israel imeangusha makombora katika eneo la kaskazini mwa ukanda wa Gaza kwa lengo la kukishambulie kile wanajeshi wa Isarel walichookiita bohari la silaha.
Msemaji wa jeshi ameeleza kuwa shambulio hilo limefanywa dhidi ya bohari ya silaha iliyoko mjini Beit Hanoun iliyokuwa na maroketi aina ya Qassam pamoja na makombora
Wakati huo huo wanamgambo wakipalestina wamefanya mashambulio ya maroketi zaidi ya ishirini pamoja na makombora dhidi ya makazi ya walowezi wa kiyahudi katika Gaza.
Wanamgambo hao wamedai kufanya hivyo kulipiza kisasi dhidi ya uvamizi uliofanywa na Israel.