GAZA:Mpaka wa Palestina na Misri wafunguliwa kwa muda
23 Septemba 2005Matangazo
Mamlaka ya Palestina imefungua kwa muda mpaka wake mkubwa na misri kwa ajili ya safari za dharura wiki mbili baada ya mpaka huo kufungwa na wanajeshi wa Israel walioondoka kwenye maeneo hayo.
Wizara ya mambo ya ndani ya Palestina imearifu kwenye taarifa yake kwamba mpaka huo wa Rafah utafunguliwa kwa saa 48 kwa wapalestina wanaotaka kwenda makazini,mafunzo au matibabu.
Maafisa wa Palestina wamesema mpaka huo utafungwa tena jumapili.
Wakati huo huo wanajeshi wa Israel wamewauwa kwa kuwapiga risasi wanamgambo watatu wapalestina wa kundi la Islamic Jihad katika ukingo wa magharibi.