1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Opresheni ya Israel dhidi ya wanamgambo wa Palestina kuendelea Gaza

6 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvf

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ameahidi kusonga mbele na opresheni dhidi ya wanamgambo wa Kipaklestina huko kaskazini mwa Gaza.

Kufikia jana jumapili watu 48 waliuwawa kufuatia opresheni ya Israel kwenye eneo hilo la kaskazini mwa Gaza kwenye mji wa Beit Hanoun.

Wapalestina wanne pamoja na wanamgambo wawili wa kundi la Hamas waliuwawa kwenye mashambulio ya hapo jana.

Opresheni hiyo ya Israel ilianza wiki iliyopita kwa lengo la kuzuia mashambulio ya kila siku ya Roketi dhidi yake kutoka Gaza.

Kwa mujibu wa Israel mashambulio hayo ya Roketi ya wanamgambo wakipalestina yanafanywa kutoka mji huo wa Beit Hanoun.