1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA:Mazungumzo juu ya kuleta mageuzi katika biashara yavunjika

25 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG4M

Mazungumzo juu ya kuleta mageuzi katika mfumo wa biashara duniani yamevunjika baada ya kufanyika kwa muda wa miaka mitano.

Wajumbe kwenye mkutano wao mjini Geneva walishindwa kufikia mapatano katika masuala ya ruzuku na ushuru .

Nchi za Ulaya zimeilamu Marekani kwa kukataa kupunguza zaidi ruzuku inazotoa kwa wakulima,wakati Marekani nayo imezilaumu Brazil na India kwa kutokuwa tayari kufikia usikizano juu ya ushuru zinazotoza katika bidhaa za viwanda.

Marekani pia imezilaumu nchi za Ulaya kwa kukataa kupunguza zaidi ushuru wa bidhaa za kilimo.

Mazungumzo juu ya kuleta mageuzi katika mfumo wa biashara duniani yalianzishwa miaka mitano iliyopita kwa lengo la kuzisaidia nchi masikini ili zinufaike na mfumo mpya.

Mkurugenzi wa shirika la biashara duniani bwana Pascal Lamy amezitaka nchi zote ziangalie upya misimao yao ili mazungumzo hayo yaweze kufufuliwa mnamo siku za usoni.