1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghasia yatanda Misri, watu 75 wauawa.

27 Julai 2013

Kiasi ya watu 75 wameuwawa katika mapigano makali nchini Misri katika maandamano makubwa baina ya mahasimu wanaounga mkono jeshi na wanaopinga kuangushwa kwa rais Mohamed Mursi,anayechunguzwa kwa mauaji.

https://p.dw.com/p/19F44
Wafuasi wa Mursi wakikimbia mabomu ya kutoa machozi
Wafuasi wa Mursi wakikimbia mabomu ya kutoa machoziPicha: Reuters

Mapambano yanaendelea katika hali inayozidi kuongezeka ya mvutano na waungaji mkono wa itikadi kali za Kiislamu wa Mursi. Mkuu wa sera wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amelaani ghasia na mauaji vilivyotokea, na kuzitaka pande zote nchini Misri kusimamisha vurugu mara moja.

Umwagikaji wa damu umeongeza hali ya wasiwasi kulikumba taifa hilo la Kiarabu lenye wakaazi wengi, na huenda hali hiyo ikachochea kuchukuliwa hatua muhimu na jeshi dhidi ya chama cha Mursi cha Udugu wa Kiislamu wiki tatu baada ya kuondolewa kutoka madarakani.

epa03802557 Egyptian opponents and supporters of ousted President Mohammed Morsi clash during a protest in the coastal cuty of Alexandria, Egypt, 26 July 2013. Egyptian authorities on 26 July ordered ousted president Mohammed Morsi to be detained for 15 days pending further investigations on charges of conspiring to carry out 'hostile acts' in the country, reported state-run newspaper al-Ahram online. Morsi's backers and opponents were, meanwhile, rallying for rival demonstrations across the country, mainly in Cairo. Scores of anti-Islamist activists were turning out at central Cairo's Tahrir Square in response to a call made by army chief Abdel-Fattah al-Sissi, who engineered Morsi's ouster. The Islamist group's followers were also on 26 July flocking to the area of Rabaa al-Adawiya, in north-eastern Cairo, joining many others who have been camping there for weeks to protest what they call a military coup against Morsi, Egypt's first democratically elected president. EPA/FAHIM TAREK
Wapinzani na wafuasi wa Mursi wakipambana mitaani mjini CairoPicha: picture-alliance/dpa

Waunga mkono jeshi

Katika jiji hilo lenye wakaazi wengi, mamia kwa maelfu ya Wamisri waliitikia wito wa mkuu wa majeshi jenerali Abdel Fattah al-Sisi kuingia mitaani na kutoa mamlaka ya kupambana na ghasia zilizotokana na kumuondoa madarakani hapo Julai 3 rais wa kwanza nchini Misri kuchaguliwa katika uchaguzi huru.

Chama cha udugu wa Kiislamu kilifanya maandamano yao, wafuasi wakimiminika na kujaza eneo linalokaliwa hivi sasa na waandamanaji ambao wako katika eneo hilo kwa muda wa mwezi sasa kaskazini ya Cairo kabla ya ghasia kuripuka. Mwandishi habari wa shirika la habari la Reuters amejionea mapambano makali ya silaha katika majira ya asubuhi ya Jumamosi kati ya majeshi ya usalama na waungaji mkono wa Mursi, ambao walivunja mawe katika eneo la wapita njia na kuwarushia polisi.

Members of the Muslim Brotherhood and supporters of ousted Egyptian President Mohamed Mursi attend Friday prayers during a rally around Rabaa Adawiya square where they are camping, in Cairo July 26, 2013. Mursi is under investigation for an array of charges including murder, the state news agency said on Friday, stoking tensions as Egypt's opposing political camps took to the streets. The banner (bottom) reads, "People do not accept coup." REUTERS/Amr Abdallah Dalsh (EGYPT - Tags: POLITICS CIVIL UNREST RELIGION)
Waandamanaji katika uwanja wa Tahrir mjini CairoPicha: Reuters

Wingu la mabomu ya kutoa machozi lilitanda hewani.

Likimnukuu afisa wa polisi ambaye hakuwa na silaha, shirika la habari la Misri, MENA limeripoti kuwa watu tisa wameuawa katika ghasia nchini humo na kiasi watu 200 wamejeruhiwa. Msemaji wa kambi inayomuunga mkono Mursi amesema kuwa waungaji mkono wanane wa chama cha Udugu wa Kiislamu wameuwawa katika mapambano karibu na eneo linalokaliwa na waandamanaji kaskazini mwa Cairo pekee, na mwingine mwingine amesema kuwa walenga shabaha waliojificha juu ya nyumba walifyatua risasi.

Idadi rasmi

Idadi rasmi ya waliofariki , wengi wao ni kutoka mji wa pili nchini Misri wa Alexandria katika pwani ya bahari ya Mediterranean , ambako mamia ya watu walipambana vikali, kwa risasi na watu waliojificha juu ya majumba wakirusha mawe kwa makundi ya watu chini.

Wengi wa wale waliouawa wamechomwa visu, mahospitali yamesema , na kiasi mtu mmoja alipigwa risasi kichwani.

Baada ya al-Sisi kuwatolea wito waandamanaji kujitokeza kwa wingi, taarifa za uchunguzi dhidi ya Mursi kuhusiana na kutoroka kwake jela mwaka 2011 zimeashiria ongezeko la dhahiri la jeshi la nchi hiyo kupambana na kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani na kundi hilo la itikadi za Kiislamu.

Shirika la habari la MENA limesema kuwa Mursi ambaye amekuwa akishikiliwa katika eneo ambalo halijulikani katika eneo la kijeshi tangu kuondolewa madarakani, ameamriwa kuwekwa kizuwizini kwa muda wa siku 15 akisubiri uchunguzi.

A member of the Muslim Brotherhood and supporter of ousted Egyptian President Mohamed Mursi holds up a mask of Mursi while gesturing during a rally around Rabaa Adawiya square, in Cairo July 26, 2013. The Egyptian army is detaining Mursi over accusations of kidnapping, killing soldiers and other charges, the state news agency said on Friday. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh (EGYPT - Tags: POLITICS CIVIL UNREST)
Kiongozi aliyeondolewa madarakani Mohammed MursiPicha: Reuters

Waziri wa mambo ya ndani aliyewekwa na jeshi , Mohammed Ibrahim, amesema ukaliaji wa eneo la mjini Cairo kwa muda wa mwezi mmoja sasa na wafuasi wa Mursi , utafikishwa mwisho hivi karibuni kwa njia za kisheria, gazeti la serikali la Al-Ahram limesema katika tovuti yake.

Egypt's Defense Minister Abdel Fattah al-Sisi is seen during a news conference in Cairo on the release of seven members of the Egyptian security forces kidnapped by Islamist militants in Sinai, in this May 22, 2013 file picture. To match Special Report EGYPT-PROTESTS/DOWNFALL REUTERS/Stringer/Files (EGYPT - Tags: MILITARY HEADSHOT POLITICS)
Jenerali Abd al-Fattah as-SisiPicha: Reuters

Wasi wasi nchi za magharibi

Kuna hali ya wasiwasi katika mataifa ya magharibi kuhusiana na hatua ya jeshi dhidi ya Mursi, ambayo imezusha ghasia za wiki kadha katika taifa hilo la Kiarabu lenye ushawishi mkubwa linalopakana na mshirika mkubwa wa Marekani Israel.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Bruce Amani