1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gladbach yaizidi nguvu Schalke, Hamburg taabani

28 Aprili 2014

Borussia Moenchengladbach imeshinda goli moja kwa sifuri dhidi ya nambari tatu kwenye ligi Schalke na kubaki na pengo la points tatu karibu na nafasi ya nne na ya mwisho ya kufuzu katika Champions League

https://p.dw.com/p/1Bpki
Fussball 1 Bundesliga FC Schalke 04 vs. Borussia Mönchengladbach am 27. April 2014 in Gelsenkirchen
Picha: Martin Rose/Bongarts/Getty Images

Gladbach wako katika nafasi ya sita na wana uhakika wa kucheza katika Europa League, lakini pia wakijitahidi wanaweza kuwafikia nambari nne Bayer Leverkusen kukiwa na mechi mbili pekee zilizosalia.

Schalke ilikosa fursa ya kujihakikishia kabisa nafasi ya kucheza champions League msimu ujao lakini wako mbele ya Leverkusen na tofauti ya points tatu. Leverkusen walitokasare ya magoli mawili kwa mawili na Borussia Dortmund.

Augsburg walipepea kwa ushindi wa magoli matatu kwa moja nyumbani dhidi ya SV Hamburg na kuyaweka hai matumaini yao ya kucheza soka la Europa League. Hamburg sasa wanakodolewa macho na kitisho cha kuondoka katika Bundesliga kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya klabu hiyo.

Ni majonzi kwa wachezaji wa SV Hamburg ambao huenda wasicheze katika Bundesliga msimu ujao
Ni majonzi kwa wachezaji wa SV Hamburg ambao huenda wasicheze katika Bundesliga msimu ujaoPicha: picture-alliance/dpa

Augsburg wako katika nafasi ya nne lakini walisonga karibu na nambari saba Mainz ambayo ni tikiti ya mwisho ya Europa League. Kuyumba yumba kwa Hamburg sasa kuna maana kuwa Werder Bremen, Hanover, Freiburg na Eintracht Frankfurt wako salama na watacheza katika Bundesliga msimu ujao.

Ni VfB Stuttgart pekee, ambayo ina pengo la points tano juu ya Hamburg katika nafasi ya 15, na vilabu vilivyo katika eneo la kushushwa daraja moja kwa moja – Eintracht Braunschweig na Nuremberg – vinavyokabiliwa na hali ya kutojua hatima yao kukiwa kumesalia na mechi mbili pekee msimu huu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman