1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guantanamo Bay, Cuba. Mlinzi wa bin Laden kufikishwa mahakamani.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3F

Wizara ya ulinzi nchini Marekani imesema kuwa madai ya kula njama na kusaidia ugaidi yametolewa dhidi ya mfungwa mmoja anayeelezwa kuwa ni mlinzi na dereva wa zamani wa Osama bin Laden.

Salim Ahmed Hamdan , raia wa Yemen , atafikishwa mahakamani baadaye mwaka huu , huko Guantanamo, kituo cha kijeshi cha Marekani.

Tangazo hilo linakuja siku chache tu baada ya mahakama kuu ya Marekani kukataa kutoa hukumu juu ya rufaa iliyotolewa na Hamdan ambayo inapingana na uhalali wa kesi za vita dhidi ya ugaidi.

Kesi hizo zimeidhinishwa na baraza la Congress mwaka uliopita baada ya mahakama kuu kukataa mfumo wa zamani wa kesi hizo uliotakiwa na utawala wa rais Bush.

Hamdan alikamatwa nchini Afghanistan mwaka 2001 baada ya kudaiwa kumsaidia bin Laden , mpangaji wa shambulio la Septemba 2001 lililofanywa na wateka nyara ndege na kushambulia jengo mjini New York na makao makuu ya wizara ya ulinzi Pentagon.