GUSAU :Watu 40 wahofiwa wamekufa nchini Nigeria
1 Oktoba 2006Matangazo
Watu 40 wanahofiwa kuwa wamekufa baada ya bwawa kusambaratika nchini Nigeria.
Habari zinasema nyumba karibu 500 zilifagiliwa mbali na maji kwenye mji wa Gusau katika jimbo la Zamfara kaskazini mwa nchi hiyo.
Gavana wa jimbo hilo amesema kuwa bwawa limepasuka kutokana na mvua kubwa.